Pichani: wakulima wa zao la mpunga eneo la kapunga 1,Mbarali mkoani Mbeya wakipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 110.7 kama fidia ya hasara iliyotokana na janga la mvua kubwa iliyoleta mafuriko na kuathiri mashamba yao.
Kampuni ya Strategis kupitia bima yake ya kilimo ” MTETEZI” imeshirikiana na Benki ya Selcom Microfinance Tanzania ambapo huikatia bima mikopo yote wanayochukua wakulima ili kujilinda na hasara za kilimo zinazoweza kuwafanya wakulima washindwe kurudisha mikopo hiyo waliokopa.
Tukio hili liliotokea siku ya alhamis November 14 lilihudhuriwa na Bwana Jabir Kigoda Afisa mtendaji mkuu wa Strategis Insurance (Upande wa bima za mali) pamoja na Afisa Mkuu wa biashara wa Selcom Microfinance bwana Isaya Mwenisongole.
Strategis inaendelea kutoa wito kwa wakulima kuhakikisha wanakatia bima miradi ya kilimo kuepuka hasara ziletwazo na majanga kama ukame, mafuriko na mvua za mawe. #Mteteziinsurance













